MWENYEKITI WA KIJIJI ALIA NA HUJUMA ZA DIWANI,MTENDAJI KUMZUSHIA KUSIMAMISHWA KAZI,YEYE ASEMA AMELETA MABADILIKO MAKUBWA,AJIVUNIA KUTAFUTA ENEO LA UJENZI WA SHULE.


MWENYEKITI wa kijiji cha Muungano Kata ya Ibindi amekanusha kauli iliyotolewa na Diwani Bw:Jastini Shinje  kuwa amesimamishwa na wananchi kuendelea na wadhifa wake katika kijiji hicho.

Shinje ameviambia vyombo vya habari kuwa Bw:Makalai Njile ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho wananchi walimkataa kwenye mkutano wa hadhara kwa madai ya kuwa chanzo cha mkwamo wa maendeleo.
Hata hivyo Bw Njile amesisitiza kuwa yeye ni mwenyekiti halali mpaka sasa kwani hajapokea barua yoyote inayotoa ufafanuzi wa sababu za kumsimamisha na kwamba anacho jua ni uelewano mdogo uliopo baina yake na diwani huyo.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa taarifa za kupotosha sanjari na hujuma za kutaka kumuundoa katika wadhifa wake ulitengenezwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho,Bw.Jastini Shinje  ambaye ni diwani wa kata ya Ibindi na wenyeviti wa vitongoji.
Wakati huo huo amesema kwa mwaka mmoja ambao amekamilisha akiwa madarakani anajivunia kuweka mikakati mingi ya maenendeleo ikiwemo kutafuta eneo la ujenzi wa shule ya msingi ambayo haikuwepo tangu uongozi ulipita.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi wamekiri kuwepo kwa migongano ya kiitikadi jambo waliloliita majipu ya mkwamo wa maendeleo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA