VIONGOZI SERIKALI ZA VIJIJI NA MITAA MANISPAA YA MPANDA KUANZA KULAMBA POSHO MWAKA WA FEDHA 2016/2017.


Mstahiki meya Manispaa ya Mpanda,Mh.Willium Philipo Mbogo ameliomba balaza la madiwani kuidhinisha mpango wa kuwapatia posho wenyeviti wa vijiji na mitaa kuanzia bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 unaotarajia kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Ombi hilo amelitoa jana kupitia kikao cha 3 cha balaza la madiwani kilichofanyika jana Manispaa ya Mpanda.
Mh.Mbogo amefikia hatua ya kutoa ombi hilo baada ya kujibu swali la mmoja wa wajumbe wa balaza la madiwani aliyetaka kufahamu ni kwa jinsi au namna gani viongozi wa serikali za mitaa na vijiji wanafikiria kwa ajili ya posho
Amesema kuwa haiwezekani wenyeviti wa vijiji na mitaa na viongozi wengine wa serikali za mitaa waendelee kutopata posho yoyoyte wakati kiongozi wa juu hawezi kutekeleza na kukamilisha kazi yoyote pasipo huyo kiongozi wa ngazi ya chini kuhusika asilimia 100.
Ametolea mfano kwenye kwenye zoezi la usafi,ambapo amesema kuwa mafanikio makubwa yametokana na jitihada za uzalendo wa viongozi hao.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amesema kuwa kiasi cha fedha kitakachopatikana kutokana na uuzwaji wa viwanja zitachangia kukamilisha asilimia 20 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Manispaa kusaidia kuwezesha maendeleo ya Serikali za mitaa na vijiji  pamoja na viongozi wake kupatiwa posho.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA