KILIO CHA WANANCHI WA MTAA WA KAMPUNI KUHUSU SHULE YA MSINGI NSAMBWE CHASIKIKA,WIKI IJAYO KUKABIDHIWA MIL.9 KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA.



Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,inatarajia kukabidhi shilingi milioni tisa kwa shule ya Msingi Nsambwe iliyopo kata ya Misunkumilo kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa mawili ya shule hiyo.

Hayo yamebainishwa na Afisa elimu shule za msingi Bw.Rashid Pilly wakati akijibu swali la Hidary Sumry ambaye ni diwani wa kata ya makanyagio aliyetaka kufahamu ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa madarasa katika shule hiyo.
Bw.Pilly amezitaja shule za msingi nyingine zitakazopokea shilingi milioni kumi kila moja wiki ijayo kwa ajili ya umaliziaji ujenzi wa miundombinu ya madarasa ni pamoja na Mkokwa na Kabwanga.
Manispaa ya Mpanda inatarajia kutoa kiasi hicho cha pesa kumalizia ujenzi shule ya msingi Nsambwe ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mpanda alilolitoa hivi karibuni akitaka Manispaa kutoa pesa kumalizia ujenzi wa madarasa yaliyo usawa wa renta.
Kwa takribani miaka miwili sasa,wanafunzi wa shule ya msingi Nsambwe wapatao zaidi ya 300 sasa ,wamekuwa wakisomea chini ya miembe huku wakipata adha ya mvua na jua.
 Hata hivyo,suala la ukosefu wa madawati na vitendea kazi kama vitabu bado ni changamoto ambapo kupitia kikao cha balaza la madiwani kilichofanyika jana,diwani wa kata hiyo amesema serikali ya kata inaendelea hushirikiana na wananchi ili kutatu baadhi ya changamoto zilizo ndani ya uwezo wao.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA