MATUKIO MAKUU 11 YA WIKI YALIYOTOKEA NDANI NA NJE YA KATAVI APRILI 4-9,2016



MPANDA-APRILI 04
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemuagiza katibu tawala wa mkoa wa Katavi Bw Paul Chagonja kufuta uongozi wa mpira wa miguu KAREFA na kusimamia zoezi la uchaguzi wa viongozi wapya baada ya kufuta uliokuwepo.
Kiongozi huyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo aliwasili Aprili 4 mjini mpanda majira ya saa 9 mchana akitokea mkoani Rukwa.
Aidha ameahidi ukarabati wa uwanja wa mpira wa miguu utakao endana na hadhi ya mkoa.
Waziri Nauye mara baada ya kuwasili jana Mkoani Katavi akitokea Mkoani Rukwa,amezungumza na wadau mbalimbali wa habari utamaduni sanaa na michezo ikiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Katavi katika ukumbi wa idara ya maji mjini mpanda.
Amesema lengo la ziara yake katika mikoa mbalimbali ikiwemo mkoani ni kutaka kuishusha wizara yake mikoani ili kutekeleza majukumu ya wizara hiyo kiurahisi.
Kiongozi huyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo amewasili mjini mpanda majira ya saa 9 mchana akitokea mkoani Rukwa.
Katika hatua nyinginea alisema kuwa ameamua wizara yake kuipeleka mikoani hususani mikoa ya pembezoni mwa nchi ili kushughulikia matatizo yaliyo chini ya Wizara yake.
Waziri Nape Aprili 6 aliondoka mkoani Katavi kuelekea mkoani Kigoma na hatimaye mkoani Kagera katika ratiba yake ya kufanya ziara katika mikoa ya pembezoni mwa nchi.

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA KUUA NA KUSUDIA KUMZIKA ATAKAYE MUUA PORINI MAHALI KUSIKOJULIKANA.
MTU mmoja mkazi wa kashaulili manispaa ya Mpanda amefikishwa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda kwa kosa la kutishia kuuwa kwa maneno.
Akisikiliza kesi hiyo hakimu mkazi Bw  Syliverster Felix Makombe amemtaja mshtakiwa huyo kuwa ni Bi Sesilia Itoela (26) ambaye  alitenda kosa hilo machi 15 mwaka huu.
Hakimu Makombe amesema mstakiwa alimtishia Bi Godiliva Ngomalala  kuwa atampiga hadi kumuua na kumzika polini kusiko jilikana.
Hata hivyo mahakama imeahilisha kesi hiyo hadi itakapo sikilizwa tena april 19 mwaka huu.

WAKAZI KIJIJI CHA KASEGANYAMA MPANDA WAIOMBA SERIKALI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI DHIDI YAO.
WANANCHI waishio kijiji cha kaseganyama kata ya  kasekese wilaya ya Mpanda wameiomba serikali kutatua mgogoro wa ardhi  unaowakabili katika eneo hilo.
Wakizungumza na mpanda radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa ni mda mrefu tangia serikali itoe agizo la kuwataka waondoke tangu mwezi disemba mwaka jana bila kuonyeshwa maeneo mbadala.
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bw.Kassimu Legi amesema wako tayari kuhama endapo watapatiwa udhibitisho wa kijiji hicho kuwa kipo au laa.
Hata hivyo mkuu wa wilaya Mh.Pazza Mwamlima amesema anafahamu suala hilo nakuwa serikali imepanga ziara ya kwenda kuzungumza na wananchi hao ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza mipaka halisi ya kijiji hicho.



KUTOKAMILIKA UJENZI WA SHULE YA MSINGI NSAMBWE WILAYANI MPANDA WANANCHI WAIANGUKIA SERIKALI.
MPANDA-April 4
BAADHI ya wakazi wa mtaa wa kampuni manispaa ya mpanda wameiomba serikali kumalizia ujenzi wa shule ya msingi Nsambwe.
Wakizungumza na Mpanda radio kwa nyakati tofauti wakazi  wameelezea kusikitishwa kwao na kutokamilika kwa ujenzi huo kama ilivyo ahidiwa na serikali kuwa ujenzi huo ungekamilika mwezi march mwaka huu.
Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Cassian Challe,amesema shule hiyo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi zaidi ya miambili wanaosomea katika mahema na kukalia matofali.
Mwaka mmoja umeisha toka manispaa ya mji wa mpanda ikili kuwepo kwa mkondo huo na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo.

Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, April 07, 2016

Na.Issack Gerald-Katavi
KIKOSI cha usalama  barabani Mkoani katavi kimesema kimefanikiwa  kupunguza ajali za barabani kwa kutumia kifaa maalum cha kupima mwendo kasi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa usalama barabani Mkoani Katavi Bw John  Mfinanga wakati akitoa takwimu za  ajali  barabarani  kuanzia mwezi  January  hadi April mwaka 2016.
Hata hivyo  amesema kuwa  kifaa hicho  kina uwezo  wa kupima madereva ambao wamelewa  wakati wakiwa barabarani.
Aidha kikosi hicho kimekuwa kinatoa elimu na kuwashauri watu  wanaotumia kilevi  kuacha kabisa wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Pia ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona dereva anaendesha kwa mwendo kasi au akiwa na dalili za kutumia kilevi ili kulinda usalama wa abiria.
Amesema kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu ni ajali nne ambazo zimetokea zikihusisha pikipiki huku katika kipindi kilichopita ajali zilikuwa zaidi ya hapo.
Aprili 07,2016

MKUU wa mkoa Meja Jeneral Raphael Muhuga amefanya ziara ya kuitembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda kwa lengo la kutazama changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Akizungumza jana na wahudumu katika hospitali hiyo mkuu huyo wa mkoa amesema,moja ya changamoto alizozibaini ni uhaba wa dawa, Madaktari,wauguzi,uchakavu wa majengo.
Jeneral Muhuga  amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi BIL.2 kwa ajili ya ujenzi wa hospital ya mkoa ili kuepusha msongamano unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la wagonjwa wawili kulala kitanda kimoja.
Aidha ametoa rai kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga  madaktali wanaotoa huduma kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya nchi.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametembelea chuo cha afya ambacho  kina lengo la kutoa mafunzo kwa wanganga wasaidizi ili kutatua tatizo la upungufu wa wanganga.
Naye Mhandisi anayejenga chuo hicho amemhakikishia Mkuu wa mkoa kumaliza ujenzi huo ifikapo mwezi juni mwaka huu.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Bw.Benard Kamande amesema Hospitali hiyo inakabiliwa na ufinyu wa bajeti kuhudumia mkoa mzima wa Katavi,ubovu wa magari ya kubeba wagonjwai pamoja na upungufu wa wahudumu 157.

AHUKUMIWA JERA MIAKA 4  AU KUTOA FAINI YA MILIONI MOJA NA LAKI MBILI KWA TUHUMA ZA KUKAMATWA NA KICHWA NA NYOKA AINA YA KOBLA NA PEMBE YA INSHA,YUPO PIA ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTISHIA KUUWA
MPANDA-Aprili 08
MAHAKAMA ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu mtu mmoja kwenda jera miaka minne au kulipa faini ya shilingi milioni moja na laki mbili.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bw Chiganga Tengwa amemtaja mtuhumiwa  kuwa ni Bw Joseph Mwananoni (70) ambaye alikamatwa na kichwa cha kobla pamoja na pembe ya insha vyenye thamani ya shilingi milioni moja.
Tengwa amesema  mshtakiwa  alikamatwa  na askari wa jeshi  la polisi katika kituo cha basi akijiaanda kusafirisha nyara hizo.
Kufuatia hukumu hiyo mahakama imetoa onyo kali  na fundisho kwa jamii kuacha kujihusisha na vitendo vya ujangiri.
Richa ya juhudi zinazo fanywa na askari wa wanyama poli kwakushirikiana na jeshi la polisi bado vitendo vya uwindaji halamu na ujangiri vinaendelea.
Wakati huo huo watu wawili wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda kwa kutuhumiwa na wizi wa katoni za soda zenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni kumi na moja mali ya Sadamu Ally.
Akisikiliza kesi hiyo hakimu mkazi Bw chiganga tengwa amewataja washtakiwa kuwa ni Ramadhani Juma na Abubaida  wakazi wa manispaa ya Mpanda.
Tengwa amesema  mnamo tarehe 13 mwezi wa 12 mwaka jana washtakiwa walikutwa na hasara hiyo na miliki wao ndipo alipo wachukulia hatua.
Ikiendelea kusikiliza ushahidi kutoka upande wa mlalamikaji mahakama imeahilisha shtaka hilo hadi litakapo tajwa tena Aprili 18 mwaka huu.

SERIKALI YAZINDUA UJENZI WA BARABARA KUTOKA MPANDA KUELEKEA TABORA KWA KIWANGO CHA LAMI KILOMITA 342.9,PIA UJENZI WA BARABARA KUTOKA MBINGA HADI MBAMBA BAY MKOANI RUVUMA NAYO WAZINDULIWA.
KATAVI-Aprili 08
SERIKALI imezindua rasmi ujenzi wa barabara ya Mpanda-Tabora yenye urefu wa kilomita 342.9 kwa kiwango cha rami ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Mpanda mkoani KATAVI  hadi Pangale Tabora.
Uzinduzi huo umetekelezwa na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja General mstaafu Raphael Muhuga,kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa katika halfa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri
Mh. Muhuga amesema Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 342.9 itauganisha kanda 3 za  nyanda za juu kusini,kanda ya ziwa na ukanda wa mashariki.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Muhuga ametoa wito kwa viongozi mbalimbali ili kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo kuzingatia ulipaji fidia kwa wakazi watakaopitiwa na mradi huo katika maeneo yao.
Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika Bi.Helene Minja amesema kuwa kiasi cha zaidi ya trilioni 2 kimetengwa kutumika katika ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni njia muhumu ya maisha ya watu wa Katavi.
Kwa upande wake Mhandisi toka TANROADS aliyekuwa mwenyekiti wa uzinduzi huo, Bw. Patrick Mfugale amesema kujengwa kwa barabara hizo kutaongeza kasi ya maendeleo.
Bw.Mfugale ametaja baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika barabara ya Mpanda kuelekea Tabora ni pamoja na Wizi.
Mbali na uzinduzi wa ujenzi wa barabara kutoka Mpanda hadi Tabora,uzinduzi huu pia umekwenda sambamba na uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay yenye kilomita zaidi ya 60.
Ufunguzi huo umehudhuliwa na viongozi Mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.Agrey Mwanri,Waheshimiwa wabunge,wenyeviti wa Halmshauri zilizopo Mkoani Katavi,Mkuu wa Wilaya ya Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Aprili 2,2016,Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifanya ziara ya kuangalia changamoto za miundombinu ya barabara mkoani Katavi ikiwa ni pamoja na kutembelea daraja la mto Koga
Ujenzi wa baraba hizi ni moja ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli ambayo aliitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ambapo pia mapema mwezi Februari mwaka 2015 wakati akiwa waziri wa ujenzi wa miundombinu alikuwa ameahidi ujenzi wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na reli kutoka Mpanda kuelekea Karema.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa michache nchini, ambayo hadi sasa haijaunganishwa na mikoa mingine kwa barabara za lami tangu mwaka 1961 Tanganyika ilipopata Uhuru.

NJE YA KATAVI
Aprili 08,MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo, Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo hivi karibuni.
Pia ameagiza fedha hizo zilizolipwa kwa watumishi hao hewa na kuiingizia hasara kubwa Serikali zirudishwe mara moja.
Akifafanua alisema katika uhakiki huo, watumishi hewa tisa walibainika katika wilaya ya Nkasi, wanane katika Manispaa ya Sumbawanga na mmoja wilaya ya Sumbawanga wakati Kalambo ikiwa haina mtumishi hewa.
Uhakiki huo unatokana na maagizo aliyotoa Rais John Magufuli baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa aliowateua, aliwaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za wananchi na sio kwenda kufanya siasa.
Pia Rais Magufuli aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika orodha ya malipo ya mshahara wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.
Zelothe alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana kilichojumuisha wazee , viongozi wa dini , watendaji wa umma na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kilichofanyika mjini hapa. Akisisitiza kuwa hajaridhishwa na uhakiki huo, hivyo akaagiza halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa watumishi.
Aliongeza kuwa aliporudi mkoani humo na kuripoti kazini katika siku yake ya kwanza ofisini alikabidhiwa kitabu chenye orodha ya watumishi wa umma wa halmashauri zote akielezwa kuwa hakuna mtumishi hewa katika mkoa wa Rukwa.

RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU WA WILAYA HAI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016.
Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.
Uteuzi huo ameufanya ikiwa ni siku moja baada ya kurejea kutoka nchini Rwanda alikokuwa akifanya ziara ya siku mbili.
 Asante kwa kuchagua P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA