RC KATAVI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA WILAYA MPANDA,ASEMA SERIKALI IMETENGA BIL.2 KUTUMIKA UJENZI HOSPITALI YA MKOA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAGONJWA.


Na.Vumilia Abel-Katavi
MKUU wa mkoa Meja Jeneral Raphael Muhuga amefanya ziara ya kuitembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda kwa lengo la kutazama changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Akizungumza jana na wahudumu katika hospitali hiyo mkuu huyo wa mkoa amesema,moja ya changamoto alizozibaini ni uhaba wa dawa, Madaktari,wauguzi,uchakavu wa majengo.
Jeneral Muhuga  amesema serikali imetenga kiasi cha shilingi BIL.2 kwa ajili ya ujenzi wa hospital ya mkoa ili kuepusha msongamano unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la wagonjwa wawili kulala kitanda kimoja.
Aidha ametoa rai kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga  madaktali wanaotoa huduma kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya nchi.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ametembelea chuo cha afya ambacho  kina lengo la kutoa mafunzo kwa wanganga wasaidizi ili kutatua tatizo la upungufu wa wanganga.
Naye Mhandisi anayejenga chuo hicho amemhakikishia Mkuu wa mkoa kumaliza ujenzi huo ifikapo mwezi juni mwaka huu.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Bw.Benard Kamande amesema Hospitali hiyo inakabiliwa na ufinyu wa bajeti kuhudumia mkoa mzima wa Katavi,ubovu wa magari ya kubeba wagonjwai pamoja na upungufu wa wahudumu 157.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA