AJALI ZITOKANAZO NA VYOMBO VYA MOTO KATAVI ZAPUNGUA.


Na.Issack Gerald-Katavi
KIKOSI cha usalama  barabani Mkoani katavi kimesema kimefanikiwa  kupunguza ajali za barabani kwa kutumia kifaa maalum cha kupima mwendo kasi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa usalama barabani Mkoani Katavi Bw John  Mfinanga wakati akitoa takwimu za  ajali  barabarani  kuanzia mwezi  January  hadi April mwaka 2016.
Hata hivyo  amesema kuwa  kifaa hicho  kina uwezo  wa kupima madereva ambao wamelewa  wakati wakiwa barabarani.
Aidha kikosi hicho kimekuwa kinatoa elimu na kuwashauri watu  wanaotumia kilevi  kuacha kabisa wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Pia ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona dereva anaendesha kwa mwendo kasi au akiwa na dalili za kutumia kilevi ili kulinda usalama wa abiria.
Amesema kuwa katika kipindi hicho cha miezi mitatu ni ajali nne ambazo zimetokea zikihusisha pikipiki huku katika kipindi kilichopita ajali zilikuwa zaidi ya hapo.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA