WANANCHI WILAYANI MPANDA WALIOMBA JESHI KATAVI KUONGEZA KASI YA KUZUNGUKIA MITAA KUIMARISHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO.


Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,limeombwa kupita mara kwa mara katika mitaa ambayo wamekuwa hawapiti mara kadhaa ili kuimarisha usalama na kukomesha udokozi wa mali za raia unaoendelea.

Ombi hilo limetolewa na baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wananchi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu udokozi wa mali za raia.
Mionogni mwa mitaa ambayo imeelezwa kuwa Polisi hawapiti mara kwa mara ni pamoja na Mtaa wa Mpadeco na mtaa wa Kasimba uliopo kata ya Ilembo mita chache kutoka Makao makuu ya jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi.
Februari 16 mwaka huu,mkaguzi msaidizi wa Polisi Wilayani Mpanda Godfrey Ndangala akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Kituo cha Polisi Wilayani Mpanda,alikiri kuwepo kwa hali ya ubomoaji wa milango,madirisha na ukataji nyavu unaosababishwa na wezi.
 Matukio ya udokozi wa mali za raia umekuwepo kwa muda mrefu wilayani Mpanda ambapo hata hivyo limepungua tofauti na ilivyokuwa kipindi cha siku zilizopita.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA