MGONJWA ALIYEMNASA KIBAO HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA MKOANI KATAVI MUUGUZI ATOROKA HOSPITALINI.


Na.Issack Gerald-Katavi
Mgonjwa aliyempiga Bi.Recho Matinya ambaye ni muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wakati mgonjwa huyo akiwa amelazwa katika Hospitali hiyo,ametoroka kutoka hospitalini hapo.
Mganga mfawidhi wa Hosptali ya Wilaya ya Mpanda Dk.Jovin Mlinda akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA amesema, mgonjwa huyo alitoroka siku moja baada ya tukio la kupigwa kwa muuguzi huyo.
Tukio la kupigwa kwa muuguzi huyo lilitokea Machi 08 mwaka huu katika wodi ya wagonjwa baada ya mgonjwa huyo kutakiwa kulala pamoja  na mgonjwa mwingine kutokana na uhaba wa vitanda katika hospitali hiyo.
Inasemekana kuwa huenda mgonjwa huyo akawa ametoroshwa na ndugu zake kwa wakati ambao ndugu huingia kuwaona wagonjwa wao kwa Dk.Jovin Mlinda amesema kuwa hakuna taarifa zinazoonesha kuwa kuna daktari alimuruhusu mgonjwa huyo kuondoka.
Mbali na tukio hilo kutokea mkoani Katavi,Machi 8 mwaka huu,madaktari katika Hospitali ya Butimba wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza, nao waligoma kutoa huduma kwa zaidi ya saa sita wakidai kunyanyaswa na kutishwa na watu wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA