KUKMBUKUMBU YA MIAKA 32 YA KIFO CHA WAZIRI MKUU MZALENDO HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE


(Na.Issack Gerald-P5 TANZANIA MEDIA)
Hayati Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli iliyopo mkoani Arusha.
Waziri Mkuu wa awamu ya 3 na 5 wa Tanzania
                 

Hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli,akafaulu kujiunga na shule ya sekondari Umbwe,hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958.
Alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961 wakati taifa letu tukufu Tanganyika likipata uhuru wake.
Kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya Maasai Land kama nilivyokwambia kwa sasa ni Monduli nah ii ikiwa ni kutokana na ufanyakazi wake uliotukuka wilayani Monduli.
Wananchi hawakuwa na budi kumchagua,wakamchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa serikali.
Hayati baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere na hatimaye akamchaguwa kuwa Naibu wa wizara ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967.
Haikuishia hapo,nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia hayati Sokoine ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa waziri Mkuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania kipindi hicho.
Kama utakumbuka mwaka 1977 ni mwaka ambao katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayotumia kwa sasa ilitungwa kwati huo ikiwa chini ya mwamvuli wa chama kimoja kwani mfumo wa vyama vingi vya siasa ulianzishwa miaka 7 baadaye yaani mwaka 1992 na kuwa na uchaguzi wa wa kwanza wa vyama vingi vya saiasa mwaka 1995 uongozi wa mfumo huo ukianzia kwa Rais wetu wa awamu ya Tatu Benjamini Willium Mkapa.

Hayati sokoine alikuwa hasa aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje hiyo ikiwa ni mwaka 1981,1983 ambapo baadaye alirudi kuendelea kama waziri mkuu wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa kwa sasa eneo hilo lilikwishabatizwa jina linguine na kuitwa Wami Sokoine mkoani Mororgoro.
Ajali hiyo ilipelekea mauti yake palepale,kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata baada ya kuachiwa huru.
Itakumbukwa kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa ndege mara baada ya kikao cha NEC,Isipokuwa hayati Sokoine ,yeye alisema wazi ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla,
 
Miongoni mwa maneno aliyoyasema mwaka 1984 mwezi April kabla ya kufariki dunia  ambayo yatakumbukwa na watnzania daima ni haya hapa.
"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"
Hayati Sokoine aliongoza vipindi viwili tofauti kuanzia
13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980 CCM na baadaye tena 24 Februari 1983 hadi 12 Aprili 1984 CCM.
Orodha ya Viongozi wa Serikali ya Tanzania
Waziri Kiongozi wa Tanganyika
Jina
Amechukua Ofisi
Ameondoka Ofisini
Chama
2 Septemba 1960
1 Mei 1961
Mawaziri Wakuu wa Tanganyika
1 Mei 1961
22 Januari 1962
22 Januari 1962
9 Desemba 1962
Nafasi Zilizoondolewa Tangu (9 Desemba 1962-17 Februari 1972)
Mawaziri Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
17 Februari 1972
13 Februari 1977
13 Februari 1977
7 Novemba 1980
7 Novemba 1980
24 Februari 1983
24 Februari 1983
12 Aprili 1984
24 Aprili 1984
5 Novemba 1985
5 Novemba 1985
9 Novemba 1990
9 Novemba 1990
7 Desemba 1994
7 Desemba 1994
28 Novemba 1995
28 Novemba 1995
30 Desemba 2005
30 Desemba 2005
7 Februari 2008
9 Februari 2008
20 Novemba 2015
Kassim Majliwa   20 Nov,2016 hadi sasa     CCM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA