DIWANI AWAMWAGIA SIFA WANANCHI WAKE USHIRIKI WA SHGHULI ZA MAENDELEO.


Na.Alinanuswe Edward
WAKAZI wakata ya makanyagio manispaa ya Mpanda wameonyesha mwamko wa ushiriki katika shughuri za maendeleo kupitia utekelezaji wa mpango wa elimu bure.

Hayo yamesemwa leo na Diwani wa kata hiyo Mh.Haidary Sumry alipokuwa akizungmzia kuhusu utekelezaji wa sera ya elimu bure.
Katika hatua nyingine Diwani huyo,amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule ya msingi Katavi kuwa ni uhaba wa madawati pamoja na vyumba vya madarasa ambapo amewaomba wadau na wananchi kwa ujumla kuguswa  na jambo hilo.
Tangu serikali ya awamu ya tano kutangaza elimu bure kumekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi.
Katika Manispaa ya Mpanda kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza ambapo mfano wa shule moja yenye wanafunzi wengi katika Manispaa yam panda ni Shule ya Msingi Nsemulwa yenye wanafunzi zaidi ya 2000 huku darasa la kwanza na chekechea pekee wakiwa zaidi ya 800.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA