DAKTARI ANAYETUHUMIWA KUSABABISHA KIFO CHA MWANANCHI KATAVI KWA KUTOMHUDUMIA AJIFUNGUA MTOTO.


DAKTARI wa zahanati ya Kapalamsenga wilayani Mpanda, anayetuhumiwa na wakazi wa kijiji hicho kusababisha kifo cha  Bi.Ana Kilangi (49) kwa kugoma kumhudumia, amejifungua salama.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpanda ,Dk Jovin Mlinda amemtaja daktari huyo kuwa ni Bi Rehema Munga aliyejifungua mtoto mwenye uzito wa kilo tatu hospitalini hapo Jumapili iliyopita.
Siku moja kabla ya kujifungua,askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka kambi ya Ikola walilazimika kuilinda nyumba yake baada ya wananchi wenye hasira kutishia kuichoma moto .
Bi Ana Kilangi kabla ya kifo chake, alifikishwa katika zahanati hiyo saa moja usiku kwa matibabu, lakini daktari huyo alikuwa tayari amelala nyumbani kwake, na kutokana na hali ya ujauzito alishindwa kwenda kumhudumia mgonjwa huyo.
Matukio ya madaktari kulalamikiwa kutotoa huduma kama inavyostahiri  kwa wagonjwa yamekuwa yakitokea hata nje ya mkoa wa Katavi ikiwemo Mkoani Mwanza.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA