WIKI YA MAJI KATAVI,WANANCHI WATAKA MAADHIMISHO YATUMIKE KUWALETEA MAJI SAFI NA SALAMA.


Na.Issack Gerald-Katavi
BAADHI ya Wakazi wa Manispaa ya Mpanda wameiomba Serikali kutatua changamoto ya maji inayowakabili katika maeneo yao.

Wakizungumza juu ya Wiki ya maji wakazi hao wamesema, wanakabiliwa na changamoto ya  uhaba wa maji safi na salama.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maji Mkoani Katavi Geraldine Mwamasangula amekiri kuwepo uhaba huo, na kufafanua kuwa  Serikali imejipanga kutatua  changamoto hiyo.
Amesema serikali iko mbioni kukamilisha ujenzi wa Mantaki 2 ya maji  ya Ikolongo yenye ujazo wa lita million moja kwa kila tanki yatakayosaidia kutatua changamoto hiyo
Aidha Mhandisi Mwamasangula amewataka wananchi kuzingatia utunzaji wa vyanzo vya maji, na kutumia maji kwa uhangalifu.
Mwezi uliopita,Mkurugenzi wa idara ya maji Mkoani Katavi Injinia Zacharia Nyanda,alikuwa amesema kuwa kuanzia mwezi machi mwaka huu,zoezi la utandazaji wa mabomba mapya utaanza ambapo kwa mjibu wa Injini huyo wa maji Mkoani Katavi mradi huo haujaanza kutokana na uhaba wa pesa.
Wiki ya maji katika mkoa wa Katavi ilizinduliwa machi 16 ambapo maadhimisho haya Kitaifa  huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 16 na kilele chacke machi 22 .

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA