WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA NIDHAMU YA WOGA,MABILIONI YAOMBWA KUIDHINISHWA KUFANIKISHA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MPANDA


Na.Issack Gerald-Mpanda
Watumishi wa umma Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kutofanya kazi kwa nidhamu ya woga na badala yake watumie taaaluma waliyoisomea.
                                       
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw.Pazza Mwamlima(PICHA NA.Issack Gerald)

Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima kikao cha kamati ya ushauri ambacho kimefanyika kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kikao ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa iadara ya maji Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine,Mkurugenzi wa Idara ya maji Mkoani Katavi Injinia Zacharia Nyanda amesema chanzo kikuu kinachosababisha maji kutopatikana kwa maji katika baadhi ya maeneo ya manispaa ya Mpanda ni uzarishaji mdogo wa maji.
Kikao hicho ambacho kimefanyika ukmbi wa idara ya maji kinawahusisha viongozi na wakuu wa idara mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi ngazi ya Wilaya na Mkoa.
Akiwasilisha taarifa katika kikoa hicho cha kupitisha mpangao wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/2017,Mchumi wa Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Kanumba,katika taarifa yake ameiomba serikali kuidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 23.8. kwa ajili ya kuekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na shughuli nyingine za kiutawala na maendeleo.
Amesema kuwa,Shilingi Bil.19.3 ni kwa ajili kwa bajeti ya kawaida na Shilingi Bil.4.4 nje ya komo wa bajeti.
Bi.Kanumba Mapato ya ndani katika Manispaa,amesema kuwa pato limeongezeka kutoka Shilingi Bil.1.9 hadi Shilingi Bil.2.3 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 18.5 ambapo ongezeko hilo limechangiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato vikiwemo  kodi ya majengo,ushuru wa zao la tumbaku,leseni za biashara,minada na ushuru wa vileo.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017,katika taarifa ambayo imesomwa na Mchumi wa Halmshauri ya hiyo Bw.Filemon Mrageri,Halmshauri ya Mpanda imeomba kuidhinishiwa Shilingi Bilioni Bil 31 Mil.584 laki moja thelathini na sita elfu mia saba na arobaini (31,584,136,740) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Hata hivyo,bajeti ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi imeonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa miongoni mwa sababu ikiwa ni utanuzi wa mipaka ya utawala na ajira mpya kwa watumishi katika Halmashauri zote za Manispaa ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho muhimu katika Halimashauri,kimeshirikisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao,wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara mbalimbali katika katika halimshauri zote,watendaji wa kata na baadhi ya viongozi kutoka Idara katika ngazi ya Mkoa akiwemo Meneja wa Idara ya Maji Mpanda Injinia Zacharia Nyanda na Meneja Mpya wa wa Kwanza wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Katavi.  

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA