WABUNGE KATAVI WACHACHAMALIA MAJI,UMEME BARABARA


Na.Issack Gerald-Bungeni Dodoma (Kuhusu Katavi).
SERIKALI imeanza mikakati ya kukamilisha miradi ya maji  ili wananchi wapate maji kama ilivyo kusudiwa.

Hayo yamejili leo bungeni mjini Dodoma baada ya mbunge wa mpanda vijijin Bw. Suleiman Moshi Kakoso na mbunge wa jimbo la Ngara Bw. Alex Raphael Gashaza kutaka kufahamu mikakati ya serikali kwa wananchi katika kuwaletea huduma ya maji.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge hao Naibu Waziri wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Gerson Lwenge waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Gerson Lwenge amesema serikali imeanza kuchukua hatua ya kuhakikisha huduma hiyo inamfikia kila mwananchi.
Mhandisi Lwenge  amesema miradi ya umwagiliaji mwaka 2015/2016 imetengewa fedha kiasi cha shilingi bilioni 53 katika kuendeleza sekta ya umwagiliaji ambayo inasimamiwa na tume ya umwagiliaji.
Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Kavuu Mkoani Katavi Bi. Pudensiana Kikwembe amehoji serikali ina mpango gani wa kuwaletea wananchi wa eneo hilo nishati ya umeme ambapo akijibu swali hilo naibu waziri wa nishati na madini Bw. Menod kalemani amesema wanaendelea na ukarabati wa miundombinu ili wananchi wote wapate nishati hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA