MWANAFUNZI SHULE YA MSINGI AFA MAJI MPANDA


Na.Issack Gerald-Mpanda

Mwanafunzi shule ya msingi Kashato aliyejulikana kwa jina la Julius Justin Albano(12) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kashato amekufa maji akiwa anavua samaki katika mto Mpanda maeneo ya Kigamboni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 03/02/2016 majira ya saa 4 asubuhi katika maeneo ya Kigamboni kata ya Nsemulwa Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
 Kamanda kidavashari amesema kuwa,tarehe 02/02/2015 majira ya saa 12:00 mama mzazi wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Prisca selemani (35) mkazi wa Kigamboni alimwagiza dukani kwenda kununua sabuni ambapo baada ya kumwagiza,yeye alielekea msibani huko maeneo ya Nsemulwa na ilipofika majira ya saa 06:00 mchana alirudi nyumbani na kukuta marehemu hayupo, ndipo alipoanza kumtafuta bila mafanikio.
Ilipofika tarehe 03/02/2016 majira ya asubuhi alipata taarifa kuwa marehemu alionekana maeneo ya pembezoni mwa mto Mpanda akiwa na watoto wenzake wanavua samaki.
Baada ya kupata taarifa hizo walianza kumtafuta maeneo hayo na walifanikiwa kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umezama chini ya maji katika mto Mpanda maeneo ya kigamboni.
Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa kitabibu kwani hapakuwa na shaka yoyote juu ya kifo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwaelimisha watoto kuacha tabia ya kwenda kucheza,kuogelea au kuvua samaki kwenye mito, madimbwi ya maji hasa wakati huu wa msimu wa mvua ili kuweza kujiepusha na matukio ya namna hii yasitokee ndani ya jamii. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA