ASASI ZA BINAFSI ZA KIRAIA NA SERIKALI ZAAGIZWA KUELIMISHA JAMII MASUALA YA SHERIA KATAVI,RAIS MAGUFULI NAYE ATOA AGIZO KALI DAR,MAHAKAMA YA MAFISADI KUJENGWA MWAKA HUU


Na.Issack Gerald-Katavi
Asasi za kiraia na zile za serikali zikiwemo vyombo vya habari, wanaharakati wa haki za binadamu wametakiwa kushirikiana kwa pamoja kuelimisha jamii juu ya kanuni zinazotumika kushughulikia kudai haki za madai na jinai kwa mjibu wa kanuni na sheria hapa nchini.
                                            

Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa  Dk Yahya Hussein kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika maadhimisho ya siku ya sheria duniani ambayo katika Mkoa wa Katavi maadhimisho haya yamefanyika katika viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Mpanda.
Kwa upande wake Farhat Seif wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoani Katavi pamoja na kuzungumza masuala mbalimbali amesema kuwa watumishi wa mahakama na wadau wengine wa sheria  wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwemo kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuepuka wananchi kujichukulia sheria mikononi kutokana na wananchi kukosa imani na vyombo vya maauzi.
Naye mwenyekiti wa Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Tanganyika Law Sciety Mh.Simon Buchur ambaye pia ni mwakilishi wa Takukuru Taasisi ya kupambana na rushwa Mkoani Katavi amesema kuwa manung’uniko ya wananchi kwa vyombo vya mahakama vitakwisha ikiwa mwananchi atatendewa haki mahakamani ipasavyo bila kucheleweshwa pamoja na kupatiwa nakala ya kesi inayomhusu mhusika ili kama ni kukata rufaa kwa mjibu wa   sheria afanye kama inavyotakiwa.
Maadhimisho haya pia yamehudhuriwa na Hakimu mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mpanda  Chiganga Tengwa ambaye pia ndiye anayekaimu mahakama ya hakimu Mkazi ya Mkoa wa Katavi,Wakili Adolf Mishanga  mwakilishi wa Shirika la Wwakimbizi la umoja wa mataifa la UNHCR Mishamo,watumishi mbalimbali wa mahakama,wadau mbalimbali wa heria na wananchi.
Hata hivyo licha ya kuwa baadhi ya wananchi walio wengi wameonesha kutotambua maana ya siku ya sheria duniani,baadhi ya waliohudhuria sherehe hizi wameeleza kujifunza mengi ambayo yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao ya kila siku ikiwemo kuzingatia msemo kuwa ‘’Kutofahamu sheria siyo kinga ya kupatiwa adhabu’’
Wakati hayo yakiwa yamejiri Mkoani Katavi,Jijini Dar es Salaa,mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Rais Dk.John Pombe Magufuli ameviagiza  vyombo vyote vinahusika katika kutoa haki kuhakikisha vinatoa haki kwa wakati na kwa wale wote wanaoharibu sifa za vyombo hivyo wachuliwe hatua ikiwa ni kiiashirio cha kuanza mwaka wa mahakama hapa nchini.
Aidha Rais ameagiza kuharakishwa kuundwa kwa mahakama ya kushughulikia mafisadi na watu wanaojihusisha na rushwa kwani hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Jaji  Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman amesema kuwa wapo katika mchakato ili kuhakikisha mahakama hiyo inafanya kazi kwa mwaka huu wa 2016.
Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni  ‘’UTOAJI WA HAKI INAYOMLENGA MTEJA,WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU.
Nchini Tanzania Maadhimisho ya siku ya sheria yalianzishwa mwaka 1996 ambapo kitaifa mwaka huu yameadhimishwa Jijini Dar es Salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa uongozaji mkuu wa Jaji  Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA