JAMII KATAVI YATAKIWA KUTAMBUA HAKI YA ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU


Na.Issack Gerald-Mpanda
JAMII wilayani Mpanda Mkoani Katavi  imetakiwa kutambua haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu kwa kuwaandikisha katika shule zinazotoa elimu maalumu kwa watoto walemavu.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA  Afisa elimu kitengo cha vifaa na takwimu wa halmashauri ya wilaya ya mpanda Bw. Amos Mwasa amesema elimu ni haki ya kila mtu, hivyo wazazi wenye watoto wenye ulemavu watambue haki ya watoto wao ya kupata elimu stahiki.
Aidha Bw. Mwasa amesema baadhi wa wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao, pasipo kuwapeleka shule na kuwanyima haki ya kupata elimu.
Amesema mwitikio wa kuandikisha watoto wenye ulemavu katika shule ya Kakora bado ni mdogo kwani mpaka sasa wameandikishwa wanafunzi wanane tu.      

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA