HAKIMU MAHAKAMAYA WILAYA YA MPANDA ATOA NENO KWA WANAKATAVI KUHUSU SIKU YA SHERIA FEBRUARI 4,2016.


Na.Issack Gerald-Mpanda
WAKAZI wa Mkoa wa Katavi wameaswa kuyatumia vizuri maadhimisho ya siku ya sheria nchini, kupata elimu inayotolewa na wadau wa sheria ili kuelewa haki na wajibu wa raia.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda radio leo,  hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mpanda Bw. Chiganga Tengwa amesema kila mwananchi anatakiwa kuzielewa sheria za nchi ili kuepuka malalamiko pindi raia atakapochukuliwa hatua za sheria.
Akizungumzia tatizo la kesi kucheleweshwa, Bw.Tengwa amesema kwa mahakama ya wilaya  mpanda tatizo hilo halipo na kwamba kesi zote husikilizwa kwa wakati unaotakiwa.
Uzinduzi wa siku ya sheria mkoani Katavi umefanyika jana katika uwanja wa kashaulili na Kauli mbiu ya mwaka huu ni  “Utoaji wa haki unaomlenga mteja,wajibu wa mahakama na wadau”
Kilele cha maadhimisho hayo yatafikia tarehe 4 mwezi huu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA