UDSM YAENDESHA KONGAMANO LA TAFAKURI YA UCHAUZI WA MWAKA 2015,MENGI YAIBULIWA.


Na.Mwandishi wetu-Dar es salaam
Watanzania wametakiwa kuacha ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake wajikite kutatua matatizo ya kitaifa.
                                                     
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jajji Joseph Sinde Warioba

Hayo yamebainishwa leo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Josefu Sinde Warioba katika kongamamno la tafakuri ambalo limefanyika Katika ukumbi wa chuo kikuu cha Dar es salaa wakijadili hoja mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu wa Tanzania  mwaka 2015.
Jaji Warioba amesema kuwa ni lazima kuondoa matatizo ya Rushwa,ukabila,udini huku akiwataka watanzania kuchagua viongozi wanaoona matatizo ya kitaifa kuliko kuchagua viongozi wanaojali masuala ya vyama vyao.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa kongamano hilo,waligusia mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu siasa kipindi cha uchaguzi mwaka 2015,nafasi ya vyombo vya habari katika uchaguzi wa mawaka 2015 katika kuripoti hali ya uchaguzi,majukumu ya viongozi wa kitaifa kama rais,mawaziri ,tume ya taifa ya Uchaguzi na katiba ya Tanzania.
Kuhusu Katiba baadhi ya wajumbe wametaka katiba ya jaji Joseph Sinde Warioba iwe ndiyo katiba itakayojadiliwa huku wakitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuwa huru ili kupata uchaguzi wa huru na haki katika kipindi cha uchaguzi.
Kongamano hilo limeshirikisha wasomi na wahitimu mbalimbali wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo mwenyekiti wa kongamano hilo alikuwa ni Jaji Joseph Sinde Warioba.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA