DAMU SALAMA YAKUSANYWA MPANDA


Na.Lutakilwa Lutobeka-MPANDA
Wizara ya afya kupitia kitengo cha damu salama Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kimewapongeza wananchi walojitokeza katika zoezi la uchangiaji wa damu huku kikiwaomba ambao hawajachangia wafanye hivyo ili kuokoa uhai wa wagonjwa.
                                                          
Damu salama iliyokusanywa

Hayo yamesemwa na mhamasishaji wa zoezi hilo Wilayani Mpanda Bi. Redgunnda Mayorwa wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA katika viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili akisema kuwa wananchi waliochangia damu jana wamepunguza tatizo la upungufu wa damu hospitalini.
Aidha Bi.Mayorwa,amesema,wanawake wameonekana kutokuwa na mwamko wa sula hilo wakati wao ndio wahanga wakubwa wa matatizo ya upungufu wa damu kwani hakuna hata mwanamke mmoja aliyejitokeza.
Naye mwenyekiti wa bodaboda Wilayani hapa Bw.Stephano Mwakapafu  amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza katka zoezi la uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa hospitalini.
Jumla ya UNITS 25 za damu zimekusanywa jana

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA