WAFANYABIASHARA WA MATUNDA SOKO LA MPANDA HOTELI WANAOUZIA CHINI WAGOMA KUOANDOKA

Na.Issack Gerald-Mpanda
Wafanyabiashara wa bidhaa katika soko la Mpanda hoteil lililopo halmashauri ya mji Mpanda wamegomea agizo lililotolewa na Mwenyekiti wa soko hilo bwana Boniphace Mganyasi la kutaka kuhamisha bidhaa zao chini na kupeleka katika vichanja vya ndani.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa hii leo katika soko la mpanda hoteil wakati wafanyabiashara wakipinga kwa nguvu zote kuondolelwa katika eneo ambalo wamekuwa wakiweka biashara zao hususan maembe,hukuwakisema ya kuwa mwenyekiti huyo amekuwa na upendeleo kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Kwa upande wake bwana Dismas Benjamin ambaye ni mmoja kati ya wafanyabiashara katika soko hilo amesema serikali inabidi iwaangalie vizuri kutokana na wao kutegemea biashara hiyo kusomesha watoto pamoja na kulea familia zao.
Akijibu tuhuma hizo bwana mganyasi amesema kuwa yeye alikuwa anatoa taarifa tu kwa wafanyabiashara kwani kuanzia kesho kutakuwa na na opresheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote walio weka biashara zao chini.
Hata hivyo wafanyabiashara hao walienda mbali zaidi na kumtaka mwenyekiti huyo ajiuzuru lakini kabla ya kujiuzuru ni lazima wajue mapato na matumizi kwa miaka minne iliyopita.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA