KUUWAWA BODABODA KATAVI,KWAWAAMSHA POLISI KATAVI,WAAMUA KUITISHA MKUTANO WA BODABODA


Na.Issack Gerald-MPANDA
Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya waendesha pikipiki Mkoani Katavi,Mkuu wa usalama barabarani ameitisha kikao kinachotarajia kufanyika kesho kujadili kwa kina suala hilo.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Ofisini kwake,Mkuu wa Usalama Barabarani Bw.Mafinanga John wakati akizungumza na  Mpanda Radio Ofisini kwake.
Kwa upande wa waendesha bodaboda Wilayani  Mpanda wameelezea  kufurahishwa na kuunga mkono hatua hiyo ya Jeshi la polisi kufanya Mkutano kujadili changamoto za waendesha Bodaboda.
Naye Kaimu katibu wa chama cha waendesha pikipiki Wilayani Mpanda,John Simtowe,amesema hatua hiyo ya polisi kuitisha mkutano huo utazaa matunda kutokana na kuwepo wigo mpana wa kujadili chanamoto zinazowakabili waendesha bodaboda hususani suala la mauaji.
Wiki iliyopita,mwendesha pikipiki mmoja mkazi wa mtaa wa kichangani amekufa baada ya kuuwawa baada ya kuchukuliwa na bodaboda huyo kumsafirisha kama abiria ambapo hata hivyo muuaji hajafahamika.
                                                              

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA