WAOMBA KIKAO CHA AMANI KATAVI


 
Picha ya pamoja kati ya wazee maarufu,viongozi wa kisiasa,dini na wafanyabisahara na Kamanda wa Polisi Mkoa ni Katavi Dhahirii Kidavashari mara baada ya kujadili mikakati ya kuimarisha amani na uasalama katika mkoa wa Katavi kuelekea uchaguzi

Na.Issack Gerald-KATAVI
Mkuu wa  Mkoani Katavi ameombwa kuitisha kikao maalumu kinachojumuisha tume ya taifa ya uchaguzi,wanasiasa na wazee maarufu Mkoani Katavi  ili kujadili namna ya kukabiliana na viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani vinavyojitkeza kwa sasa kuelekea uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu.

Ombi hilo limetolewa leo katika kikao maalumu cha tatu kinachojumuisha wazee maarufu ,wanasiasa na wafanyabiashara kikao ambacho kimefanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi kujadili mustakbali wa amani Mkoani Katavi kipindi cha kampeni.
Kwa upande wake kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Rashid Mohamed ametoa wito kwa wakazi MKoani Katavi kutounga mkono kauli zinazoweza kuligawa taifa.
Wakati huo huo Oktoba 16 imependekezwa kufanyika kikao cha Mkuu wa Mkoa huku kingine cha Kamanda Polisi Mkoa kikipangwa kufanyika Oktoba 19 mwaka huu


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA