SIKU YA MWALIMU YAZUNGUMZWA NA CWT KATAVI


NA.Issack Gerald-MPANDA
Chama cha walimu CWT Mkoa wa Katavi kimesema kimefanikiwa katika masuala mbalimbali yakiwemo udhibiti wa wizi wa mishahara ya walimu,ujenzi wa benki ya mwamili tangu kuanzishwa kwake.

Siku ya mwalimu duniani ni inaadhimishwa kiduniani kila mwaka ifikapo Oktoba 05.
Siku hii inalenga zaidi kuangalia masuala yanayowahusu walimu katika maeneo yao ya kazi ikiwemo utatuzi wa changamoto zinazowakabili walimu  bila kusahamu kuboresha mafanikio wanayoyapata walimu, haya yote yakifanyika kwa ajili ya kuinua kiwango cha mtoto ili tupate taifa la leo na kesho lililo imara na lililoelimika huku suala la ushindani kielimu kati ya nchi hususani nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki likishika kasi kuumiza vichwa vya watanzania kuingia katika ushindani wa ajira.
P5 TANZANIA imezungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu CWT Mkoani Katavi John Mshota na kutaja changamoto zinzowakabili kwa sasa ni pamoja na malimbikizo ya posho na mishahara ya walimu.
Pamoja na kuzungumzia chanamoto zinazowakabili Mshota ametaja baadhi ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa CWT Mkoani Katavi ni pamoja na kushiriki ujenzi wa benki ya mwalimu hapa nchini na kudhibiti wizi wa mishahara ya walimu kwa njia ya mtandao wa benki.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA