WAKAZI WILAYA MPYA YA TANGANYIKA WAOMBA HUDUMA ZA JAMII


 
Wakazi Wilaya mpya ya Tanganyika wakizungumza na P5 TANZANIA Wilayani hapo

NA.Issack Gerald-TANGANYIKA
Wakazi katika Wilaya Mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameiomba serikali ya Mkoa wa Katavi kuongeza huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo afya na Ofisi za Watumishi wa Umma  katika kata ili kuondokana na adha ya kupata huduma umbali mrefu.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo wakati wakizungumza na P5 TANZANIA kuhusu chanamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Aidha wamesema mamlaka zinazohusika Mkoani Katavi zifanye mpango wa mgawanyo wa utawala kata hadi kata ili wajue eneo wanakotakiwa kupata huduma za jamii.
Baadhi ya maeneo yanayounda Wilaya Mpya ya Tanganyikia ni Pamoja na Tarafa ya Karema na kata zake.
Tangazo la kupatikana Wilaya ya Tanganyika  lilitolewa mwezi Agosti mwaka huu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa wakati wa kuvunja balaza la mawaziri.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA