TUME YA UCHAGUZI MANISPAA YA MPANDA YAONYA WATAKAOBAINIKA KUANDIKA MAJINA YA WATU NA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA KINYUME CHA SHERIA


Na.Issack Gerald-MPANDA
Tume ya taifa ya uchaguzi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imewataka watu wanaojipitisha katika mitaa mbalimbali ya Manispaa hiyo kuorodhesha majina na namba za kitambulisho cha Mpiga kura kuacha tabia hiyo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa uchaguzi Manispaa ya Mpanda Bw.Clavery Reginald wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu kukithiri kwa matukio ya kukamatwa kwa baadhi ya watu wakisemekana kufanya kazi hiyo.
Uchaguzi wa Tanzania unatarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu ukishirikisha vyama mbalimbali vya siasa Tanzania vikiwemo nane katika ngazi ya Urais.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA