UKATA WA PESA TANAPA KATAVI CHANZO CHA KUSHINDWA KUANDAA MAADHIMISHO SIKU YA TEMBO KIMKOA


NA.Issack Gerald-Katavi
Uongozi wa hifadhi ya taifa ya wanyama ya Katavi umeshindwa kuandaa maadhimisho ya siku ya tembo kutokana na ukata wa kifedha ulipo katika shirika hilo mkoani hapa.

Hayo yamebainishwa leo na mhifadhi Mkuu idara ya ujirani mwema katika hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Katavi Bw.David Kadomo wakati akizungumza na P5 TANZANIA kuhusu siku ya tembo kitaifa ambayo imeadhimishwa leo.
Aidha amesema elimu inaendelea kutolewa kwa jamii kupambana na kutokomeza ujangili dhidi ya  tembo na wanyama wengine.
Maliasili na Utalii ikishirikiana na Shirika la Uhifadhi Duniani WWF ofisi ya Tanzania  kwa pamoja wanaadhimisha siku ya tembo kitaifa mwaka huu kwa kujadili na wadau mbali mbali kuhusu kuwaokoa wanyama Tembo kupitia vyombo vya habari hapa nchini.
Maadhimisho haya yanatokana na mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa kuzuia biashara ya Wanyamapori na viumbe walioko hatarini kutoweka uliofanyika mwaka 2010 katika mji wa Doha nchini Quatar.
Nchi 37 zilizojaliwa kuwa na tembo barani Afrika zilikutana, na kupitisha mpango mkakati wa kuhifadhi tembo barani Afrika  Ambapo Mwaka uliofuatia wa 2011 Tanzania ilianza kutekeleza mpango mkakati maalum wa uhifadhi wa Tembo.
Tanzania inasifika kwa kuwa na utajiri mkubwa wa wanyamapori barani Afrika na Ulimwenguni kote,ikiwa  ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na rasilimali nyingi asili.
Katika kuhakikisha kuwa wanyamapori hususani Tembo wanalindwa, Tanzania imetenga zaidi ya asilimia 24 ya ardhi yake kwa ajili ya uhifadhi.
Kipaumbele cha Mpango Mkakati wa uhifadhi ni pamoja na; kulinda shoroba za wanyamapori hususani Tembo; kupunguza migogoro kati ya wananchi na Tembo; kufanya tafiti za uhifadhi wa tembo na kushirikisha wadau mbalimbali katika kuhifadhi Tembo.
Serikali imekua ikifanya shughuli za uhifadhi wa wanyamapori kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kiserikali, mashirika ya kimataifa kama WWF, taasisi zisizo za kiserikali, wafanyabiashara, taasisi za kidini na wananchi kwa ujumla. 


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA