MWANAMKE AKAMATWA NSIMBO AKIANDIKA MAJINA NA NAMBA ZA VIPARATA


Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la SALOME MAKALA, miaka 56, mkulima, mnyamwezi mkazi wa Mwenge Kitongoji cha Legezamwendo septemba 21 siku ya Jumatatu majira ya saa 4:00 kamili usiku alikamatwa akiwa anaorodhesha majina ya wanakijiji wa kijiji cha Mwenge Kata ya Nsimbo Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi kwenye daftari kwa kuandika majina yao na namba za vipalata vyao (kadi ya mpigakura).

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari alisema kuwa Jeshi la Polisi lilipokea taarifa toka kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Nsimbo kwa tiketi ya  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) GERALD KITABU kuwa kuna mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la SALOME MAKALA ameonekana akiorodhesha majina ya wananchi wa eneo la Kijiji cha Mwenge pamoja na namba zao za vipalata.
Kufuatia taarifa hiyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema walifanikiwia kufika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha kumfikisha kituo cha Polisi Nsimbo.
Katika mahojiano ya awali, mtuhumiwa alieleza kuwa lilikuwa ni zoezi la kukusanya taarifa za wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (CWT) wa eneo lao ili kuwa na kumbukumbu.
Hata hivyo, upelelezi wa shauri hili bado unaendelea.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA