WAZAZI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUWAFICHUA WATAKAOTOZA MICHANGO ILIYOPIGWA MARUFUKU SHULENI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
Na.Issack Gerald
Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano
kwa halmashauri hiyo kuwabaini watu watakawatoza michango ya shule iliyopigwa
marufuku ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Jengo la Manispaa ya Mpanda |
Aidha,Mwalimu
Pili amesema muda wowote wanatarjia kuendesha msako wa watoto ambao hawajapekwa
shule ili wazazi wachukuliwe hatua za kisheria kwa kumnyima mtoto haki ya
kielimu.
Kauli
ya Afisa elimu wa Manispaa ya Mpanda inakuja ikiwa ni kufuatia taarifa za hivi
karibuni zilizosambaa mitaani kuwa kuna baadhi ya shule za Manispaa ya Mpanda
ambazo zinakataa kumsajili mwanafunzi wa chekechea na darasa la kwanza mpaka
alipe kiasi cha fedha kilichopangwa.
Manispaa
ya Mpanda ina jumla ya shule 34 za serikali ambazo zinatakiwa kusimamiwa ili
kuhakikisha agizo la elimu bila malipo lililotolewa na Rais Dkt.John Magufuli
linatekelezeka.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments