AHUKUMIWA VIBOKO



MAHAKAMA  ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imemuhukumu  Paschal Kabagi (18)  kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na  hatia ya kumbaka  mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anzyesoma Kidato cha Kwanza katika shule ya Sekondari Nkomolo wilayani humo.

Akisoma hukumu  hiyo mwishoni mwa wiki jana,hakimu wa mahakama hiyo,Ramadhani  Rugemalira  alisema  kuwa kwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa  hilo akiwa na umri wa miaka  17 ataadhibiwa kwa kucharazwa viboko sita ili iwe  fundisho kwa wengine wenye tabia kama yake.
Awali  mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi , Hamimu Gwelo alidai mahakamni hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo  Januari 12 , 2016 majira  ya saa  mbili asubuhi katika kitongoji cha Uwanja wa Ndege kilichopo mjini Namanyere wilayani Nkasi.
AlidaI mahakamani hapo kuwa  wakati akitenda kosa hilo mshitakiwa  alikuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nkasi.
Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alimvizia mwanafunzi huyo wa kike kwenye mahindi wakati akienda shule ndipo alipo mshika kwa nguvu na kisha kumuangusha chini na kumbaka.
Mshtakiwa alijitetea kwa kuiomba mahakama  imsamehe kwa kuwa  hakujua kuwa alichokifanya kilikuwa kosa kisheria utetezi uliopingwa na mwendesha masthaka na kisha mahakama hiyo ikaamua kutoa hukumu hiyo.
Hukumu hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopitia
Chanzo:Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA