MTANGAZAJI MCHEZAJI AFARIKI DUNIA
Mtangazaji na mchezaji mkongwe wa Uingereza mwenye heshima kubwa,Jimmy Armfield amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 82 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
Pamoja na kuichezea mechi 569 Timu ya Blackpool enzi zake,
pia alikuwa Nahodha wa England mara 15 katika mechi 43 alizochezea Simba
Watatu.
Baada ya kuwa kocha wa timu za Leeds na Bolton, Armfield
akahamia kwenye utangazaji na kujivunia heshima kubwa akiwa mchambuzi wa BBC
Radio 5 Live. Na Familia yake imethibitisha kifo chake kilichotokea Trinity
Hospice mapema asubuhi ya leo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments