WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA BILA HOFU
SERIKALI mkoani Rukwa imewataka waandishi wa habari mkoani humo kuyaandika na kuyatangaza mambo mazuri na changamoto zilizopo bila kuhofia mtu yeyote kwani maendeleo ya mkoa huo yatapatikana kwa kuyatangaza mambo yaliyomo katika mkoa huo bila hofu.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo
aliwaambia waandishi wa habari wa mkoa huo jana wakati akizindua zoezi la
upandaji miti milioni sita lililofanyika juzi katika mji wa Matai wilayani
Kalambo.
Alisema kuwa waandishi wa habari ni
wadau wakubwa wa maendeleo ya mkoa huo hiyo wanawajibu wa kuandika mambo mazuri
na mabaya yaliyopo katika mkoa wa Rukwa kwani kushindwa na kufanikiwa kwa mkoa
huo nao kunawahusu.
Wangabo alisema kuwa waandishi wa
habari wanatumia kalamu katika kuchangia maendeleo hivyo wajue wanajukumu la
kuandika mazuri na changamoto ili mkoa upige hatua kwani wakikaa kimya mkoa
ukikosa maendeleo nao itawagharimu.
Alisema kuwa yeye binafsi yupo tayari
kuona mkoa wake ukitangazwa kwa mazuri pamoja na changamoto zake kwani ndiyo
fursa ya kupiga hatua,na kazi hiyo waandishi wanapaswa kuifanya kwa kuzingatia
misingi ya taaluma yao.
Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waandishi
wa habari kutembea vijijini kuandika habari za uharibifu wa mazingira pamoja na
kuhamasisha wananchi wajitume katika kilimo cha kisasa na ufugaji wenye tija
kwani mkoa huo unahitaji maendeleo.
Awali akimkaribisha mkuu huyo wa
mkoa, mkuu wa wilaya ya Kalambo Juliath Binyura alisema kuwa wananchi wa wilaya
ya Kalambo wamejipanga katika kutekeleza zoezi la upandaji miti kwani wanatambua
kuwa miti ni uhai.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya
hiyo ipo tayari kuwadhibiti watu watakao baininika kuharibu mazingira kwakuwa
serikali inatumia fedha nyingi na muda hivyo ni lazima waone thamani ya miti.
Binyura alisema kuwa kwakuwa mkuu wa
mkoa amekwisha zindua kampeni ya upandaji miti wananchi wameipokea na
wanahakikisha watafikia lengo kwa asilimia mia moja kwani wao ni wakulima na
wanahitaji mvua ambayo haiwezi kupatikana bila kuwepo misitu.
Chanzo:Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments