LIGI YA WANAWAKE KUANZA KUTIMUA VUMBI FEBRUARI 24
LIGI
ya Wanawake ya Serengeti Premier Lite hatua ya nane bora inatarajia kuanza
kutimua vumbi Februari 24, 2018 kwenye viwanja vine.
Mchezo
kati ya Kigoma FC na Simba Queens utakaochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika
ndio utakuwa mchezo rasmi wa ufunguzi.
Mechi
nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya ufunguzi ni Panama watakaokuwa
nyumbani Uwanja wa Samora kucheza na Evergreen,JKT Queens wakicheza dhidi ya
Alliance kwenye uwanja wa Mbweni.
Mechi
nyingine ni ile nitakayowakutanisha Baobab na Mlandizi Queens utakaochezwa
kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kabla
ya kufika kwenye hatua hiyo,ligi hiyo inayodhaminiwa na bia ya Serengeti
Premier Lite kinywaji murua na chenye ubora wa juu ilianzia kwenye hatua ya
makundi ikichezwa kwenye Kituo cha Dar Es Salaam kilichotumia Uwanja wa Karume
na Kituo cha Arusha kilichotumia Uwanja wa General Tyre.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments