MOROCCO YAZINDUA KAMPENI YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA 2026
Morocco imezindua kampeni yake ya
kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca.
Taifa hilo la Afrika kaskazini ambalo limewasilisha ombi lake
la tano kuandaa fainali hizo,linakabiliwa na ushindani mkali kutoka ombi la
pamoja linaloshirikisha Canada,Mexico na Marekani.
Mwenyekiti wa ombi hilo Moulay hafid Elalamy amesema Morocco
itaonyesha mchezo mzuri zaidi katika kombe hilo la dunia.
Uamuzi wa atakayeandaa kombe hilo unatarajia utafanywa juni
13 mwak huu katika mkesha wa kombe la dunia la mwaka 2018 mjini Moscow.
Taifa hilo la Afrika kaskazini limefeli katika maombi yake
manne miaka 1994,1998,2006 na 2010.
Mwaka wa 2010,mchuano huo uliandaliwa na Afrika Kusini huku
bara hili likiandaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia.
Morocco inataka kubadili hayo yote na imemteua Elalamy,
waziri wa serikali kuongoza ombi hilo huku aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho
la soka Afrika Hicham El Amrani akiwa afisa mkuu mtendaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments