ISMAIL SUMA ALIYEDAKIA YANGA,SIMBA AFARIKI DUNIA BURUNDI
KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania,Ismail Suma aliyedakia klabu za Simba na Yanga za Dar es Salaam amefariki dunia leo mjini Bumbura,Burundi.
Kwa
mujibu wa ndugu wa marehemu,Juma Athumani Salum ni kwamba Suma amefariki leo
asubuhi mjini Bujumbura baada ya kusumbuliwa na maradhi ya ini na figo kwa muda
mrefu.
Suma
alikuwa anacheza nchini Burundi alikokwenda akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) ambako alicheza pia akitokea nyumbani Tanzania.
Mpango
wa awali ulikuwa ni kuurejesha mwili wa marehemu kwa mazishi kwao mkoani
Tabora,lakini imeshindikana kutokana na wafiwa kutokuwa na fedha za kutosha
gharama za kusafirisha maiti.
Na
kwa sababu hiyo wamepanga kumzika ndugu yao huyo huko huko mjini Bujumbura
jioni ya leo.
Suma
aliibukia Kariakoo United ya Lindi mwaka 1998 na akadaka hadi mwaka 2000
alipohamia Yanga SC kabla ya baadaye kuchezea timu nyingine kadhaa,ikiwemo
Simba SC na African Lyon wakati bado inaitwa Mbagala Market ingawa ilivyopanda
Ligi Kuu akaondoka.
Mungu
ampumzishe kwa amani marehemu Ismail Suma. Amin.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments