MGOYI KUSIMAMIA MECHI YA AFC LEOPARDS NA TIMU YA MADAGASCAR KOMBE LA SHIRIKISH
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ahmed Iddi 'Msafiri' Mgoyi kuwa Kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa klabu kati ya AFC Leopards ya Kenya na Fosa Juniors ya Madagascar.
Kwenye
mchezo huo waamuzi wote wanatoka nchini Somalia ambapo mwamuzi wa kati ni
Abdulkadir Artan Omar,mwamuzi msaidizi namba moja Ali Mohamed Mahad,mwamuzi
msaidizi namba mbili Ahmed Abdullah Farah wakati mwamuzi wa akiba ni Hassan
Mohamed Hagi.
Mgoyi
ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya utendaji wa TFF walioteuliwa hivi karibuni
kuwa makamishna wa mechi zinazoandaliwa na CAF kwa mwaka 2018 mpaka mwaka 2020
wengine ni Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura,Amina Karuma na Sarah Tchao.
Aidha
Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia naye mbali ya kuteuliwa kwenye kamati ya
mashindano ya fainali za Africa kwa wachezaji wanaocheza ndani CHAN tayari
amechaguliwa mara mbili kusimamia mechi za CHAN zinazoendelea nchini Morocco.
Alisimamia
mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha Wenyeji Morocco na Mauritania Januari 13,
2018 na mchezo wa pili uliochezwa jana Januari 22,2018 kati ya Namibia na
Zambia.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments