WAKAZI TABORA WATAKIWA KUACHA KUTUMIA DAWA KWA MAZOEA
Wananchi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wameshauriwa kujenga utamaduni wa kuhudhuria
katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuacha kutumia dawa kwa mazoea.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa zahanati ya Moravian Milumbani,Dkt
Lameck Kisulila amesema matumizi ya dawa bila utaratibu maalumu ni chanzo cha
magonjwa nyemelezi mwilini na hata kusababisha vifo.
Dkt.Kisulila ameitaka
jamii kuwa na desturi ya kupima afya wanapougua kwa sababu itasaidia kubaini
aina ya ugonjwa na tiba inayohitajika hatua itakayowasaidia kupunguza madhara
mengine mwilini yanayotokana na usugu wa dawa.
Kwa upande wao baadhi
ya wananchi wa mjini Tabora wamesema wanalazimika kutumia dawa bila kupima afya
zao wanapougua kutokana na hali ngumu kiuchumi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments