WAKULIMA MKOANI KIGOMA WAPEWA ELIMU YA KUENDESHA KILIMO BORA
Halmashuri
ya Kigoma vijijini ikishirikiana na Shirika la maendeleo la vijana Tanzania la
nyakitonto limeendesha semina ya kilimo cha mihogo,maharage na mahindi katika
kata ya Nkungwe halmashuri ya Kigoma Ujiji.
Kwa
mjibu wa katibu washirika la Nyakitonto la mendeleo ya vijana wa Tanzania Teoneste
Tereba amesema wakulima wengi wadogo
wadogo wamekua na desturi za kulima kilimo cha mazoea kwa kutumia mbegu ambazo zisizokuwa
na ubora ikiwa ni pamoja na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi
ya mbolea jambo.
Aidha
Tereba amesema hali hiyo imesababisha itasaidia kuboresha kipato,uhakika wa chakula
na hali za wakulima wa maharage mahindi na mhogo kwa mkoa wa kigoma kuwa katika
ubora.
Kwa
upande wao Mikidadi Mbaruku ambaye afisa kilimo halmshauri ya Kigoma vijijini na
Silyvesta Mchafu ambaye ni afisa kilimo kata ya Nkungwe wamesema watakuwa bega
kwa began a wakulima hukuwa wakiwashauri wakulima kutumia elimu wanayopewa
katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo.
Kwa
upande wao wakulima wa mazao hayo,wamelipongeza shirika hilo na kusema kuwa
elimu amabyo wameipata itawasaidia kuboresha kilimo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments