MANCHESTER CITY YAMUONGEZEA MKATABA DE BRUYNE NA KUMPA MSHAHARA KAMA WA SANCHEZ
Manchester City imeamua kumuongeza kiungo wake wa pembeni Kevin De Bruyne mkataba wa miaka mitano na nusu.
De Bruyne atakuwa akipokea mshahara wa
jumla ya pauni 350,000 kwa wiki sawa na ule anaolipwa Alexis Sanchez
aliyejiunga na Manchester United akitokea Arsenal.
Lakini mgawanyo wa De Bruyne ni pauni
280,000 ya mshahara kwa wiki pamoja na bonas ya 70,000.
Kiungo huyo wa pembeni mwenye kazi
alikuwa akiwaniwa kwa karibu na klabu maarufu duniani ya Real Madrid na
inaonekana City wamefanya hivyo kuhakikisha anabaki.
Kwa mkataba huo,sasa De Bruyne atabaki
Manchester City hadi mwaka 2023.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments