BEKI WA KAGERA SUGAR MIKONONI MWA POLISI KAGERA
Beki wa timu ya Kagera Sugar
inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bra Juma Nyossoa anashikiliwa na Jeshi la Polisi
mkoani Kagera kutokana na tuhuma za kumshambulia kwa ngumi shabiki hadi
akazirai.
Taarifa zinaeleza,Nyosso alimshambulia
shabiki huyo mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya jana kati ya Kagera na Simba
kwenye Uwanja wa Kaitaba na wageni wakashinda kwa mabao 2-0.
Wengi wanaojadili wamekuwa wakisisitiza
tabia mbaya za kibabe za Nyosso zinapaswa kukomeshwa.
Lakini wengine nao wamekuwa wakihoji
kama shabiki huyo alikuwa sahihi kumtukana Nyosso na inaelezwa alimsogelea hadi
karibu akitoa maneno ya kashfa.
Mjadala huo unaonekana kuelemea kwa
Nyosso kwa kuwa kuna mifano ya kufanya vitendo vya kihuni uwanjani.
Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani
Kagera Josefu Olomi amesema mpaka sasa wanamshkilia mchezaji huyo kwa ajili ya
mahojiano na Nyosso anatarajia kufikishwa mahakamani mara baada ya mahojiano
kukamilika.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments