HALMASHAURI YAAGIZWA KUJENGA MWALO
MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani humo kutafuta fedha ili ijenge mwalo wa Nankanga katika ziwa Rukwa utakao wasaidia wavuvi kufanya biashara ya samaki na utakuwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa halmashauri hiyo.
Agizo hilo alilitoa mwishoni wa wiki
jana wakati alipokuwa akifanya ziara ya kukagua makambi ya wavuvi wa samaki
katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu uliotokea wilayani
humo tangu mwezi Novemba mwaka jana ambapo usababisha vifo vya watu nane na 270
kuugua ugonjwa huo.
Alisema kuwa ufukwe uliopo katika
makambi ya wavuvi ya Nankanga katika ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga linafaa
kwaajili ya kujenga mwalo ambapo wavuvi watakuwa wanafanya biashara ya samaki
na kisha halmashauri kupata fedha kwa kutoza ushuru.
Alisema kuwa wilaya hiyo imejaliwa
fursa nyingi ambazo kama zikitumika ipasavyo zitaongeza makusanyo na
halmashauri itapata fedha nyingi na itaweza kuwahudumia wananchi ili waaweze
kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili.
Alisema kuwa nilazima itafutwe
namna fedha zipatikane haraka na mwalo huo ujengwe kwakuwa wananchi wanahitaji
huduma nzuri kwani ni jukumu la watendaji kuzitambua fursa zilizopo na
kuzitumia ipasavyo.
Awali akitoa taarifa ya ugonjwa wa
kipindupindu katika halmashauri hiyo Kaimu mkurugenzi ambaye ni Mganga mkuu wa
wilaya hiyo Fani Musa alisema kuwa kipindupindu kimedhibitiwa licha ya kuwa
bado jitihada zinahitajika kutoa elimu ya afya kwa wavuvi.
Alisema kuwa changamoto iliyopo ni
kutotumia maji safi na salama kwani baadhi ya wavuvi wanakataa kutumia maji
yanayotibiwa kwa dawa aina ya waterguard kwamadai kuwa hayana radha.
Chanzo:Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments