AGIGO KALI WILAYANI TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando ameiagiza kukamatwa kwa watu waliowazuia wananchi 160
katika kijiji cha Kaseganyama kata ya Kasekese kufanya shughuli za kilimo
katika maeneo halali.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho Muhando amesema serikali ya kijiji hicho kwa kushilikiana na serikali ya
wilaya kwa pamoja waliamua kutenga hekari 1280 baada ya wananchi hao kukubali
kuondoka katika maeneo ya hifadhi jambo ambalo halijafanikiwa kutokana na
vitisho wa kikundi hicho.
Aidha katika kukabiliana na uhalifu ametoa siku kumi na nne
kwa watu wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha katika ofisi za
watendaji na vituo vya polisi vya wilaya hiyo kabla ya msako kuanza.
Katika ziara hiyo pia amekagua na kushiriki na wanachi katika shughuli za ujenzi wa shule ya sekondari Simbwesa
na shule ya sekondari Kasekese ambazo zipo katika hatua ya renta.
Ziara hiyo
ambayo aliifanya mwishoni mwa wiki iliyopita iligusia pia masuala ya kutoa
elimu kuhusu sera ya elimu bila malipo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments