MWAKA WA FEDHA 2018/2019 MANISPAA YA MPANDA KUKUSANYA ZAIDI YA BIL.26.8
Na.Issack Gerald
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Mkoani Katavi inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 26.8 katika mwaka
wa fedha 2018/2019 ambapo kati ya kiasi hicho mapato ya ndani yanarajia kuwa
Shilingi bilioni 2.4.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango wa
Manispaa hiyo Bi.Mary Luhulula wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa
fedha 2018/2019 kupitia kikao maalumu cha baraza la madiwani cha Manispaa ya
Mpanda ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa.
Aidha Bi.Luhulula pamoja na mambo
mengine amesema mwaka 2017/2018 ilikusanywa shilingi bilioni 10.4 badala ya
shilingi bilioni 27.4 iliyokuwa imeidhinishwa ambapo imepanga kubuni vyanzo vya
mapato ili kupata fedha ili kuchochea maendeleo.
Kwa upade wake Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mpanda Bw.Deodatus Kangu amesema baadhi ya tozo kurejeshwa serikali
kuu ikiwemo kodi ya ardhi,mazao,mabango ya matangazo ya kijamii na baadhi ya
ushuru kufutwa kumesababisha Hamlashauri ya Manispaa ya Mpanda kutofikisha
asilimia 50 ya makusanyo ya mapato.
Hata hivyo Stendi Mpya ya kisasa
inayotarajia kufunguliwa hivi karibuni,malipo ya papo kwa papo katika hospitali
ya wilaya,Bima za afya na madawa.
Hapo kesho inatarajiwa kuchaguliwa
kamati maalumu itakayosimamia ukusanyaji mapato katika Manispaa ya Mpanda ili
kuchochea kasi ya kushghulikia utatuzi wa changamoto zinazokwamisha maendeleo
na masuala mbalimbali ya kijamii.
Kwa mjibu wa Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Mbogo Kikao kinatarjia kuendelea kesho ili
kujadili hoja ya matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2017.2018.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments