CAF YAWASILI TANZANIA KUFANYA UKAGUZI SIMBA NA YANGA
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) itafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa klabu (Club Licensing) kwenye upande wa miundo mbinu.
CAF watafanya
ukaguzi huo wa kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo
unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo mbinu.
Wakati wa miaka kadhaa ya kuzindua mfumo huo wa leseni kwa vilabu ni wazi changamoto kubwa kwenye Bara la Africa imekuwa ni vigezo vya miundo mbinu ambayo kwenye baadhi ya viwanja vinavyotumika wakati wa mashindano imekuwa ikitoa taswira isiyo nzuri kwa mashindano ya CAF.

Kwa
mwaka huu 2018 wameandaa ukaguzi kutembelea klabu zote zitakazoshiriki hatua ya
makundi kwenye mashindano ya vilabu ya CAF wakijielekeza kwenye kiwango na
ubora wa viwanja vya kucheza mechi na viwanja walivyochagua kwa mazoezi.
Caf
watachagua kundi la wakaguzi watakaotembelea kwenye klabu za kila mwanachama
wake ili kukusanya ripoti itakayowasilishwa na moja kati ya ripoti hiyo ni
miundo mbinu ya Uwanja,ripoti itakayothibitisha kama uwanja umefikia kwenye
mahitaji ya juu ya kutumika kwa mechi za CAF.
Viwanja
ambavyo havitakidhi mahitaji hayo ya juu hautaidhinishwa kutumika kwa mashindano
na hautatumika kwa mchezo wowote wa hatua hiyo ya makundi kwa mashindano ya
klabu kwa mwaka huu 2018.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments