SHUGHULI ZA KIBINADAMU MKOANI TABORA ZATAJWA KUWA CHANZO CHA UTORO SHULENI
Shughuli za kilimo,ufugaji na uelewa mdogo kwa baadhi ya
wazazi wa wilaya ya SIKONGE mkoani TABORA ndiyo chanzo cha utoro wa wanafunzi
na kushuka kwa kiwango cha ufaulu wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya SIKONGE,PERES
MAGIRI amesema katika wilaya hiyo kuna jamii ya wafugaji ambao wanaishi mbali
na huduma za kijamii zikiwemo shule, na hivyo kusababisha wanafunzi kushindwa
kuhudhuria masomo.
Kwa upande wake,Afisa Elimu wa wilaya
ya SIKONGE,HILLALY BITWALE amesema tatizo la utoro wilayani humo siyo kubwa
sana na mahudhurio ya wanafunzi yanaridhisha
MAULID JUMA ni mmoja wa wanafunzi
watoro sugu wilayani SIKONGE amesema hapendi kwenda shuleni kwa sababu
anayofundishwa na walimu hayaelewi
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi
LEMBELIkata ya KIPANGA wilayani SIKONGE,ALLY ABDI amesema wamekuwa
wakiwahamasisha wanafunzi kujua umuhimu wa elimu ili kupambana na tatizo la
utoro
Kufuatia wilaya ya SIKONGE kuwa ya
mwisho kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana,serikali ya wilaya
hiyo imesema ina mpango mkakati wa kuwaita wadau wa elimu wakiwemo
walimu,wazazi na wananchi ili kupanga mikakati itakayowasaidia kuinua ufaulu wa
wilaya hiyo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments