WAZIRI MKUU AWASILISHA TAARIFA YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA SERIKALI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mpa akufikia Februari 2018 Serikali ya Awamu ya Tano imeanzisha viwanda vipya 3,306.
Ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma,wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.
Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika viwanda kwa kutoa vivutio vya kodi na visivyo vya kodi kwa wawekezaji mahiri wa kuendeleza na kuboresha miundombimu wezeshi kama vile barabara,reli,bandari, umeme na maji.
Aidha Waziri Mkuu amelieleza Bunge kuwa mikoa na Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya viwanda na kwamba katika mwaka 2018/2019,Serikali itatoa kipaumbele katika kutekeleza miradi ya kielelezo,uanzishwaji wa kanda maalum za kiuchumi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda.
Akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa sekta ya hifadhi ya jamii kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda,Waziri Mkuu amesema pamoja na miradi mingine NSSF na PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wanatekeleza mradi mkubwa wa uzalishaji wa sukari mkoani Morogoro.
Waziri Mkuu alisema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo Juni 2017,ajira za moja kwa moja 780 na ajira zisizo za moja kwa moja  24,000 ikijumuisha wakulima wadogo wa mbegu na kilimo cha nje zimezalishwa.
Akifafanua kuhusu ujenzi wa barabara kuu,Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kuboresha mtandao wa barabara nchini ambapo katika kipindi cha Julai 2017 hadi Februari 2018,ujenzi wa Km.776.45 za barabara kuu kwa kiwango cha lami umekamilika na Km. 1,760 zinaendelea kujengwa huku barabara zenye urefu wa Km.17,054 zikikarabatiwa katika kipindi hicho.
Kuhusu ujenzi wa madaraja,Waziri Mkuu alisema madaraja ya Kilombero na Kavuu ujenzi wake umekamilika na kwamba ujenzi unaoendelea hivi sasa ni wa madaraja ya Sibiti,Mto Mara,Lukuledi,Ruhuhu,Momba na Mlalakuwa ambapo madaraja mengine 996 katika maeneo mbalimbali nchini yamekarabatiwa.
Kuhusu jitihada za Serikali kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam,Waziri Mkuu alisema hadi kufikia Februari 2018,ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la TAZARA ulikuwa umefikia asilimia 70 na ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo umeanza.
Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuliarifu Bunge juu ya uanzishwaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Roads Agency – TARURA) kwa lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji na kuongeza kasi ya wananchi kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu aliliomba Bunge likubali kupitisha shilingi. 143,618,762,698 zikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2018/2019 ambapo shilingi 74,527,321,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 69,091,441,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Vilevile,Waziri Mkuu aliliomba Bunge liidhinishe shilingi 125,521,100,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo shilingi 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 8,315,613,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA