RC KATAVI AZINDUA VIKAO VYA KIELIMU ATOA MAAGIZO KWA WARATIBU WA ELIMU


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amewaagiza viongozi mbalimbali wa elimu mkoani Katavi kuhakikisha wanashirikiana na wadau wa elimu katika maeneo yao ili kutatua tatizo la Mkoa wa Katavi kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa elimu ya msingi,kidato cha nne na sita.
Miongoni mwa viongozi ambao wamelengwa na agizo la Mkuu wa Mkoa ni pamoja na waratibu elimu kata,wakuu wa shule,walimu wakuu,bodi na kamati mbalimbali za shule.
Muhuga ambaye alikuwa mgeni rasmi ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa vikao vya wadau wa elimu Mkoani Katavi uzinduzi ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Azimio Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 1000,taasisi mbalimbali binafsi,wazazi,walezi na wakuu wa idara Mkoa na Manispaa ya Mpanda.
Awali akiwasilisha taarifa kwa mgeni rasmi,Kaimu katibu tawala Mkoa wa Katavi Ernest Hinju ambaye pia ndiye Afisa elimu Mkoa amesema vikao hivyo vinavyoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa vinalenga kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazosababisha ufaulu wa wanafunzi kuendelea kuporomoka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Nzyungu amesema halmashauri inaendelea inaendeklea kutatua changamoto mbalimbali za kielimu katika Manispaa ya Mpanda ikiwemo ukarababti na ujenzi wa miundombinu ya shule kama madarasa ambapo mpaka sasa vyumba vya madarasa viapatvyo 26 vipo katika hatua mbalimbali za kukamilika katika shule zenye uhaba wa madarasa.
Nao wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi,wazazi,walezi, walimu,taasisi binafsi,viongozi mbalimbali wa dini na siasa ambao wameshiriki katika uzinduzi wa vikao hivyo wamesema ili mkoa wa Katavi ufanye vizuri katika mitihani ya taifa,inatakiwa kuwepo madarasa ya kutosha shuleni,stahiki mbalimbali za walimu kulipwa kwa wakati,watoto kulelewa katika maadili mema na kuongezwa idadi ya walimu shuleni.
Vikao hivyo vinatarajiwa kuwa saba ambapo vitafanyika katika halmashauri za Mlele,Nsimbo,Mpimbwe,Mpanda na Manispaa ya Mpanda ambapo kilele cha vikao hivyo kitafanyika Aprili 16 mwaka huu katika kijiji cha majimoto Halmashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlelele.
Mkoa wa Katavi kwa mwaka 2014,2015 na 2016 ulikuwa ukishika nafasi tatu za juu kitaifa kwa mitihani ya shule za msingi na sekondari lakini kwa matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2017 umeporomoka na kushika nafasi ya 9 kitaifa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA