WANANCHI NSIMBO WAOMBA KUBORESHEWA HUDUMA YA MAJI DIWANI AKATAA KUWEKA WAZI MIPANGO

Wananchi wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili wananchi waondokane na tatizo la kutofanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kupoteza muda mrefu wkifuatilia maji.
Wamesema serikali imekuwa ikisema itaongeza mabomba ya maji ambapo mpaka sasa hakuna mipango inayotekelezwa kadri siku zinavyosonga mbele licha ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Nsimbo na Diwani wa kata hiyo kutoa ahadi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Daud Peter Nyasio amekiri hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho kuwa mbaya ambapom amesema visima viwili vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi zaidi ya elfu tatu wa kijiji hicho wanaotakiwa kuapa maji.
Hata hivyo Reward Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na Kapalala ameiambia Mpanda Radio kuwa hana jambo lolote la kuzungumza na chombo cha habari kuhusu suala la maji katika kata ya Kapalala kwani kila wanapoomba pesa serikalini hazitolewi kama inavyotakiwa.
Kwa mjibu wa Mh.Sichone,kuna zaidi ya shilingi milioni 400 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maji katika kata ya Kapalala zilizotakiwa kuletwa katika kata hiyo mpaka sasa hazijatolewa na hali inayompatia wakati mgumu wa kuzungumza namna ya kutatua tatizo la maji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA