ACT-WAZALENDO KATAVI WATOA MAAZIMIO MIGOGORO YA ARDHI KATAVI

Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimeazimia kuishinikiza serikali kuchukua hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili  wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Joseph Mona ambaye ni Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Katavi akizungumza katika mkutano wa chama hicho amesema kikao hicho kilichofanyika jana kililenga kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyoshughurikia migogoro ya ardhi inayoendelea kufukuta.
Mona ametaja baadhi ya kero za wananchi zimetokana na serikali kuchukua baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa madai kuwa maeneo hayo  yalikuwa katika hifadhi za misitu.
Aidha Mona ametaja baadhi ya maeneo yenye migogoro kuwa ni pamoja na vijiji vya Litapunga,Luhafwe,Sitalike,Ugalla, Kanoge na Mpanda Ndogo.
Hivi karibuni Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa wameambatana na viongozi wa kijiji cha Sitalike pamoja na wananchi wa kijiji cha Sitalike walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kwa lengo la kuzungumza naye ili kutafuta hatima ya haki ya wananchi walifukuzwa katika maeneo yao ilihali serikali ilikosea yenyewe kuwaondoa wananchi kimakosa katika vijjiji ambavyo wananchi wanadai kuwa vilisajiliwa tangu enzi za kuanzishwa kwa vijiji mwaka 1974.
Mwaka 2017 mwezi Agost mwaka jana,mamia ya wananchi katika vijiji vya Mgorokani,kata ya Stalike na Kijiji cha Nsambwe Kata ya Kanoge waliondolewa katika makazi yao kwa madai ya kukaidi maagizo ya serikali yaliyokuwa yakiwataka kuhama katika vijiji hivyo kwa madai ya kuwa ni hifadhi za misitu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA