WADAU WA ELIMU WACHANGIA ZAIDI SHILINGI MIL.152 KWA AJILI YA SEKTA YA ELIMU


Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimechangwa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika mkoani Katavi,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhaga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda Mjini,ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Salehe Muhando pamoja na mambo mengine amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Naye Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Suleima Kakoso baada ya kuchangia komputa kwa shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu,amezishauri halmashauri Mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa maendeleo walioko ndani na nje ya halmashauri zao ili washiriki kuleta maendeleo.
Miongoni mwa mafanikio ya harambee hiyo ni pamoja na Komputa 24 Zenye thamani ya shilingi milioni 48,mifuko ya simenti 2281 ya Shilingi milioin 41,058,000,vitanda 25 vya aina ya dabodeka vyenye thamani ya shilingi 5,000,000,Malumalu boksi 200 za shilingi 5,000,000,Bando 1530 za bati zenye thamani ya shilingi 30,400,000.
Vitu vingine ni Fedha taslimu shilingi 400,000,Fedha ahadi Shilingi 17,400,000,Kokoto kubwa Tan 14 za Shilingi 520,000 na Kokoto Vumbi tan 14 za Shilingi 160,000
Wadau wa elimu ambao wameshiriki wanatoka taasisi za kifedha,wafanyabiashara,madiwani halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara wilayani Tanganyika,wakulima, pamoja na watu binafsi na idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya 200.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA